Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran katika masuala ya kimataifa, Ali Akbar Welayati, amesema kuwa uzoefu, maono ya kimkakati na moyo wa kimapinduzi wa Meja Jenerali Mohsen Rezaei vitakuwa nguzo muhimu katika kulinda usalama na maslahi ya kitaifa ya Iran.
Mwanachama wa Baraza la Utambuzi wa Maslahi ya Mfumo wa Iran, Jenerali Mohsen Rezaei, amesema Mlango wa Hormuz ni njia ya kimataifa inayotumiwa na mataifa mbalimbali na hakuna sababu kwa Marekani kuingilia suala linalohusu nchi za eneo hilo.