Ayatullah Jawadi Amuli, akitoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia kwa Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani (RA), ameeleza kuwa tukio hilo ni msiba mzito na tukio lenye huzuni kubwa katika historia.
Kauli hiyo inaonesha ukubwa wa pengo lililoachwa na marehemu katika ulimwengu wa Kishia na nafasi yake muhimu katika elimu ya Fiqhi na mafundisho ya Ahlul-Bayt (AS).
Mwenyezi Mungu amrehemu mwanazuoni huyo mkubwa na amjaalie makazi mema katika Pepo. Amina.
Sheikh Ridhiwani Mjenjwa, Mudir wa Markazi ya Imam Ali (a.s) Mkoani Kigoma, ametoa nasaha kwa akina mama waliohudhuria msiba wa mmoja wa waumini katika Kijiji cha Kasuku, Barabara ya Tisa, akisisitiza kuwa kifo ni hakika isiyoepukika kwa kila Mwanadamu. Amehimiza umuhimu wa kutubu, kutekeleza wajibu kwa Mwenyezi Mungu na wanadamu, kuacha madhambi, kufanya matendo mema na kujiandaa kwa safari ya Akhera kabla mauti haijamfikia mtu.