Mamia ya Mazuwwari na wakazi wa mji wa Qom walishiriki hafla ya kupandisha Bendera Nyeusi ya maombolezo ya Imam Hussein (AS) juu ya Kuba la Haram ya Hazrat Fatimah Masoumeh (SA), kuashiria kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Muharram na kumbukumbu ya Mashahidi wa Karbala.
Kitengo cha Forodha na Mipaka kinachohusiana na Idara ya Mahusiano ya Umma cha Ataba Tukufu ya Husseiniyya, ambacho kimepewa majukumu haya, kina uzoefu wa zaidi ya miaka 8 katika uwanja huu na kimekuwa kikifanya kazi kwa ufanisi mkubwa hata katika mazingira magumu zaidi ili kuhakikisha kuingia kwa maashura mjini Karbala kunafanyika kwa utaratibu na urahisi.