16 Juni 2026 - 14:48
Bendera ya Maombolezo ya Imam Hussain (AS) Yapandishwa katika Haram ya Hazrat Fatimah Masoumeh kuukaribisha Mwezi wa Muharram

Mamia ya Mazuwwari na wakazi wa mji wa Qom walishiriki hafla ya kupandisha Bendera Nyeusi ya maombolezo ya Imam Hussein (AS) juu ya Kuba la Haram ya Hazrat Fatimah Masoumeh (SA), kuashiria kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Muharram na kumbukumbu ya Mashahidi wa Karbala.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA-, Bendera ya maombolezo ya Imam Hussain (AS) imepandishwa rasmi juu ya Kuba la Haram Tukufu ya Hazrat Fatimah Masoumah (sa), ikiwa ni ishara ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Muharram.

Sherehe hiyo ilifanyika Jumatatu jioni, tarehe 15 Juni 2026, katika ua wa Imam Reza(as)  -Courtyard- huku ikihudhuriwa na umati mkubwa wa mazuwwari na wakazi wa eneo hilo. Hafla hiyo ilijaa mazingira ya huzuni, dua na kuwakumbuka Mashahidi wa Vita vya Karbala wakiongozwa na Imam Hussein (AS).

Kupandishwa kwa bendera nyeusi ni desturi inayofanyika kila mwaka katika maeneo matakatifu ya Kiislamu kuashiria mwanzo wa kipindi cha maombolezo ya Muharram, Mwezi unaokumbusha kujitolea, uadilifu na kusimama dhidi ya dhuluma kulikodhihirishwa na Imam Hussain (AS) katika tukio la Karbala.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha