Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Balozi Mkuu wa Iraq katika mkoa wa Kermanshah magharibi mwa Iran, Saadoun Al-Saadi, ametangaza kuwa makundi mbalimbali ya wananchi wa Iraq yako tayari kushiriki katika sherehe za mazishi ya kiongozi mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Al-Saadi pia alibainisha kuwa mipango imeandaliwa ili kurahisisha usafiri wa washiriki kupitia mipaka ya mkoa huo, akisisitiza umuhimu wa uratibu kati ya pande zote mbili.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, balozi huyo alikutana jana Jumanne na gavana wa Kermanshah ambapo alizungumzia pia mradi wa reli unaounganisha Kermanshah na Baghdad.
Amesema kuwa mradi huo wa reli umebuniwa ili kurahisisha usafiri wa mahujaji na wageni, huku akibainisha kuwa amewasiliana na gavana wa Diyala ambaye ameonesha nia kubwa ya kutekelezwa kwa mradi huo kutokana na manufaa yake ya kiuchumi kwa mkoa huo.
Your Comment