Mwangaza

  • Umuhimu wa Qur'an Tukufu katika Maisha yetu kama Wanadamu

    Umuhimu wa Qur'an Tukufu katika Maisha yetu kama Wanadamu

    Kila Aya katika Aya za Qur’an ni chimbuko la mwangaza, muongozo na rahma, kwa hiyo mwenye kutaka mafanikio ya milele na kuokoka katika dunia yake, basi ni juu yake kushikamana na kitabu cha Mwenyeezi Mungu (s.w) usiku na mchana na kuzifanya Aya za Qur’an Tukufu kuwa mfano katika kumbukumbu zake na kituo cha fikra zake ili awe katika mwangaza wa Mwenyeezi Mungu (s.w).