Rais wa Mahakama ya Juu alieleza katika sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Hazrat Fatima (S) na heshima ya mama na Siku ya Mwanamke, kwamba: katika mafundisho ya Uislamu, mwanamke ni kama “Reihana” (maua ya harufu nzuri) na maua yanayopaswa kulindwa na kutunzwa zaidi. Mtazamo huu na mazungumzo haya yana tofauti dhahiri na mafundisho ya Magharibi ambayo huona mwanamke kama bidhaa inayopaswa kuonyeshwa au kutumika.