Kiongozi huyo wa kidini wa Shia Pakistan alisisitiza kuwa leo hii, rushwa, ukosefu wa sheria na usimamizi mbovu ndizo zimeenea kote katika eneo la Gilgit-Baltistan. “Wananchi wanajiona wapo peke yao, wamenyimwa haki na hawana pa kutegemea. Endapo hali hii itaendelea, ghadhabu ya wananchi inaweza kubadilika na kuwa dhoruba kubwa ambayo mzigo wake utabebwa na watawala pekee,”
Sheikh Eid aliwapa wanafunzi nasaha kuhusu umuhimu wa kujitahidi katika masomo yao na kusisitiza nafasi ya elimu ya dini katika kujenga jamii yenye maadili mema.