Gazeti la Washington Post katika uchambuzi wake limeandika kuwa iwapo Democrats watapata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani katika uchaguzi wa katikati ya muhula, Donald Trump kwa vitendo atageuka kuwa “Rais wa kipindi cha mpito”, huku akikabiliwa na vikwazo zaidi katika kuendelea na kipindi chake cha urais.
Waandamanaji wanaopinga vita walikatiza kikao cha Seneti ya Marekani wakati wa kusikilizwa kwa maelezo ya Waziri wa Ulinzi, Pete Hegseth, wakionyesha picha za wanafunzi waliouawa katika mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran.