Ushahidi wa Riwaya za Kisunni: Shia pia wametaja kuwa baadhi ya maelezo kuhusu tukio la shambulio la nyumba ya Bibi Fatimah (a.s.) na Imam Ali (a.s.) yanapatikana hata katika baadhi ya vitabu vya Kisunni, na wamekusanya riwaya zaidi ya 84 kutoka kwa wanazuoni wa Kisunni kuhusu tukio hilo (kama ilivyokusanywa katika al-Hujūm ʿalā Bayt Fāṭimah (a.s).
Imam al-Baqir (a.s.) amesema: “Anayesema Tasbih ya Fatimah az-Zahra (a.s.) kisha akaomba maghfirah, atasamehewa. (Tasbih hiyo inaposomwa na mja) Ni mia moja kwa ulimi wake, lakini ni elfu moja katika mizani.”