Kampuni ya CinnaGen ya Iran imepata mafanikio makubwa baada ya dawa yake ya Zandoriah (teriparatide) kuidhinishwa kuuzwa katika nchi 27 za Umoja wa Ulaya pamoja na nchi tatu za EEA, hatua inayochukuliwa kuwa mafanikio muhimu kwa sekta ya dawa na teknolojia ya afya ya Iran.
Ayatollah Khamenei katika kikao na Rais pamoja na Baraza la Mawaziri alisisitiza juu ya umuhimu wa 'kutawala kwa hali ya kazi, juhudi na matumaini' dhidi ya 'hali ya si vita wala amani'