Wakati ambapo Waislamu wa Kisunni wameshindwa kufikia mwafaka juu ya mgombea mmoja, hatima ya urais wa Bunge la Iraq imefungamana zaidi kuliko wakati mwingine wowote na maamuzi pamoja na hesabu za kisiasa za Waislamu wa Kishia na vyama vya Kikurdi.
Spika wa Bunge alisema: Marekani inawagawa umma wa Kiislamu katika pande mbili — upande mmoja ambao unapaswa kushambuliwa na kukaliwa, na upande mwingine ambao unapaswa kukubali “Amani ya Ibrahimu” na kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni. Hakuna nchi yoyote ya Kiislamu inapaswa kujiruhusu kuanzisha uhusiano na adui wa Uislamu na Waislamu.