Naibu wa Kitengo cha Utamaduni, Jamii na Hija wa Mkoa wa Khorasan Razavi, Hojjatoleslam Ali Asgari, amesema kuwa idadi ya mazuwwari katika siku za mwisho za mwezi Safar imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kwa kuzingatia likizo zinazokaribia, inatarajiwa kuwa idadi ya mazuwwari itafikia takriban milioni 8.
“Kauli yenye nguvu zaidi ni hii kwamba kusikia (kusikiliza) sauti ya Mwanamke asiyekuwa Mahram, maadamu si kwa ajili ya tamaa, starehe au maslahi, ni jambo linaloruhusiwa (linajuzu). Vivyo hivyo kwa Mwanamke, ikiwa hakuna hofu ya fitina, anaweza kusikika na Wanaume wasio mahram kwake".