Katika taarifa yake muhimu na ya kina, Katibu Mkuu wa Jukmuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (as) -ABNA - amelaani matusi na vitisho vya hivi karibuni dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kushukuru misimamo yenye nuru ya viongozi na wasomi wakuu (Marajii) wa kidini duniani.
Marajii Wakuu wa Taqlid katika Ulimwengu wa Kishia, Ayatollah: Sistani, Makarem Shirazi, Nouri Hamedani, Javadi Amoli, Sobhani na Shabiri Zanjani wameshutumu katika taarifa tofauti matamshi ya udhalilishaji ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.