Taurati
-
Je, Taurati imebadilishwa? Angalia jibu la Qur’an hapa!
Kuhusu taarifa (maelezo) ya Qur’an Tukufu kuhusu ubadilishaji wa maneno ya Taurati, kuna mjadala wa kiitihadi kama ifuatavyo: 1. Mtazamo maarufu (ushahidi unaoonekana wazi kabisa katika Quran) Watafiti wengi na wafuasi wa mtazamo huu wanaona kwamba Qur’an inazungumzia ubadilishaji wa maneno kwa uwazi jabisa. Qur’an inataja maneno yaliyopinduliwa au kuharibiwa na baadhi ya Watu wa Kitabu (Ahlul-kita'bi): «يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَوَاضِعِهِ» (An-Nisa 46) Hapa (kwa mujibu wa Aya hiyo Tukufu) , ubadilishaji huo unahusiana na maneno yenyewe, na si tafsiri tu. 2. Mtazamo wa wapinzani (Mukhalifuna) Wao wanasema kuwa Qur’an inazungumzia ubadilishaji wa maana, si maneno ya kifasihi: Wanasema kuwa maneno ya msingi hayajabadilishwa, lakini maana au tafsiri potofu ndizo zilizobadilishwa au kutumika vibaya. Hii inaitwa ubadilishaji wa maana (tafsiri) badala ya ubadilishaji wa maneno.
-
Kufunga (Saumu) Kabla ya Uislamu:
Saumu kabla ya Uislamu inasemekana kuwa ilidumu kwa zaidi ya Mwezi mmoja. Ilikuwa ni Miezi mingapi na kwa nini ilikuwa ndefu?
Tunawaona Mayahudi na Wakristo wakifunga kwa namna mbali mbali hadi zama za sasa, ima kwa kujizuia kula nyama au maziwa au kula na kunywa kabisa kwa mujibu wa Hadithi, kufunga (Saumu) katika Mwezi wa Ramadhani haikuwa wajibu kwa nyumati zilizopita, bali waliokuwa wakifunga Saumu ni Mitume (Manabii) wao pekee (a.s), hao ndio waliokuwa wakifunga Mwezi wa Ramadhani.