25 Machi 2025 - 00:07
Saumu kabla ya Uislamu inasemekana kuwa ilidumu kwa zaidi ya Mwezi mmoja. Ilikuwa ni Miezi mingapi na kwa nini ilikuwa ndefu?

Tunawaona Mayahudi na Wakristo wakifunga kwa namna mbali mbali hadi zama za sasa, ima kwa kujizuia kula nyama au maziwa au kula na kunywa kabisa kwa mujibu wa Hadithi, kufunga (Saumu) katika Mwezi wa Ramadhani haikuwa wajibu kwa nyumati zilizopita, bali waliokuwa wakifunga Saumu ni Mitume (Manabii) wao pekee (a.s), hao ndio waliokuwa wakifunga Mwezi wa Ramadhani.

Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-; Kuhusu kufunga (au ibada ya Saumu) katika Dini zilizopita, inasemwa katika kamusi ya Biblia: Kwa ujumla, nyakati zote kati ya kila Madhehebu na kila Taifa na Dini, ilikuwa ni jambo la kawaida wakati wa kuingia huzuni na shida zisizotarajiwa... Watu wa Kiyahudi mara nyingi walikuwa wakifunga wakati walipokuwa wakipata fursa ya kuonyesha kuhitajia msaada na unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, na kuungama dhambi zao, ambapo walikuwa wakionyesha yote hayo kwa njia ya kufunga na kutubu, ili kupata radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu[1].

Saumu kabla ya Uislamu inasemekana kuwa ilidumu kwa zaidi ya Mwezi mmoja. Ilikuwa ni Miezi mingapi na kwa nini ilikuwa ndefu?

Kauli hii  «الَّذِینَ مِنْ قَبْلِکُمْ» | "Waliokuwa kabla yenu" kutoka katika Aya hii Tukufu:

«کُتِبَ عَلَیْکُمُ الصِّیامُ کَما کُتِبَ عَلَى الَّذِینَ مِنْ قَبْلِکُمْ»[2].

"Mmeandikiwa (mmewajibishwa) kufunga kama walivyowajibishwa (walivyoandikiwa) kufunga wale waliokuwa kabla yenu ili mpate kuwa wachamungu "[2].

Inatumika kutujulisha kwamba Nyumati za watu zilizopita zilikuwa na taratibu (au mila) na dini.

Hata hivyo, si wote watu wote wa nyumati (hizo zilizopita), na Qur’an Tukufu haifafanui nyumati hizo za watu ni zipi, lakini kitu ambacho tunaweza kukifahamu na kinachotokana na dhahiri ya sentensi hii: « ... کَما کُتِبَ» ni hiki kwamba nyumati za watu zilizotajwa  zilikuwa ni nyumati za watu wa wenye mila na dini ambao walikuwa wakifunga. Na kutoka katika Taurati na Biblia, vitabu hivi viwili vilivyopo mikononi mwa Mayahudi na Wakristo, hakuna ushahidi wowote unaoonyesha wajibu wa kufunga Saumu kwa nyumati hizi mbili za Mayahudi na Wakristo, isipokuwa katika vitabu hivi viwili kuna Aya zinazosifu Saumu na kuiona (au kuichukulia Saumu) kuwa ni (ibada) kubwa (na adhimu).

Hata hivyo, tunawaona Mayahudi na Wakristo wakifunga kwa namna mbali mbali hadi zama za sasa, ima kwa kujizuia kula nyama au maziwa au kula na kunywa kabisa kwa mujibu wa Hadithi, kufunga (Saumu) katika Mwezi wa Ramadhani haikuwa wajibu kwa nyumati zilizopita, bali waliokuwa wakifunga Saumu ni Mitume (Manabii) wao pekee (a.s), hao ndio waliokuwa wakifunga Mwezi wa Ramadhani.

Imepokewa kutoka kwa Hafs kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) kwamba alisema:

"Muumba (Mwenyezi Mungu) hakuifanya Funga (Saumu) ya Ramadhani kuwa ni wajibu kwa nyumati zilizopita".

Msimuliaji (Mpokezi) aliuliza: Kwa hivyo ni yapi makuudio ya Aya hii Tukufu inayosema: 

Saumu kabla ya Uislamu inasemekana kuwa ilidumu kwa zaidi ya Mwezi mmoja. Ilikuwa ni Miezi mingapi na kwa nini ilikuwa ndefu?

«یا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا کُتِبَ عَلَیْکُمُ الصِّیامُ کَما کُتِبَ عَلَى الَّذِینَ مِنْ قَبْلِکُمْ».

"Enyi Mlioamini! Mmeandikiwa (mmewajibishwa) kufunga kama walivyowajibishwa (walivyoandikiwa) kufunga wale waliokuwa kabla yenu...".

Imam Sadiq (a.s) akasema: “Kufunga (saumu) katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kulikuwa ni wajibu kwa Mitume (Manabii) pekee, na ndio maana ni Umma pekee wa Kiislamu uliopata ubora wa juu zaidi ya wafuasi wote wa Tauhidi, na ukawekwa kwenye kiwango sawa na Mitume (Manabii) wengine katika kutekeleza wajibu huu”[3].

Pia, ndani ya Qur'an Tukufu, kumetajwa kisa cha funga (Saumu) ya Nabii Zakaria (a.s) na kisa cha Saumu (Funga) ya Sayyidat Maryam (s.a).

Mbali na Qur'an, suala la Saumu pia limepokewa kutoka kwa watu wasiokuwa na dini, ni sawa pia na ilivyopokewa kutoka kwa Wamisri wa kale, Wagiriki, Warumi, na hata wapagani wa India hadi leo kiasi kwamba kila mmoja wao alikuwa na mfungo (saumu) na bado ana mfungo kwa ajili yake, bali inaweza kusemwa kwamba ibada na njia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia saumu ni miongoni mwa mambo yanayoamriwa na maumbile (fitrah) ya (asili ya) Mwanadamu.[4]

Saumu kabla ya Uislamu inasemekana kuwa ilidumu kwa zaidi ya Mwezi mmoja. Ilikuwa ni Miezi mingapi na kwa nini ilikuwa ndefu?

Rejea:

[1]. Mostafavi, Hassan, Tafsir Roshan, Juzuu 2, Ukurasa wa 372, Kituo cha Uchapishaji wa Vitabu, Tehran, 2013.

[2] Suratul-Baqarah, Aya ya 183.

[3]. Sheikh Sadouq, Fadhail al-Ash'huri al-Thalatha, Mtafiti (Mhakiki) na Msahihishaji: Irfanian Yazdi, Gholamreza, 124, Davari Bookstore, Qom, 1396 AH.

[4] Tabatabai, Sayyid Mohammad Hossein, Al-Mizan, iliyotafsiriwa na Mousavi Hamdani, Sayyid Mohammad Baqir, Juzuu. 2, Ukurasa wa 7 na 8, Ofisi ya Machapisho ya Kiislamu, Qom, 1374 Hijria Shamsia.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha