Tunawaona Mayahudi na Wakristo wakifunga kwa namna mbali mbali hadi zama za sasa, ima kwa kujizuia kula nyama au maziwa au kula na kunywa kabisa kwa mujibu wa Hadithi, kufunga (Saumu) katika Mwezi wa Ramadhani haikuwa wajibu kwa nyumati zilizopita, bali waliokuwa wakifunga Saumu ni Mitume (Manabii) wao pekee (a.s), hao ndio waliokuwa wakifunga Mwezi wa Ramadhani.
Sheikh Mselem: "Mayahudi walikuwepo Madina. Lakini walileta ukorofi na kibri, wakawa wakivunja makubaliano waliyokuwa wakiingia na Mtume (s.a.w.w). Mtume (s.a.w.w) akawatandika na kuwatimua kutoka katika Bara Arabu">