6 Mei 2025 - 01:30
Kwa nini Mashia wanatoa Salam za Krismasi kwa Wakristo?! | Pata jawabu maridhawa la swali hilo

Katika maisha ya Mtume wetu Muhammad (saww) ambaye ndiye Kiongozi wetu sisi kama Waislamu, bali Kiongozi wa walimwengu wote, tunapata mifano mingi ya uhusiano mwema na Wakristo, bali watu wote wasiokuwa Waislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA

Maulana Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C),  amenyoosha maelezo yake ya msingi na mazuri  yanaendana na mafundisho ya Kiislamu kuhusu kuishi kwa amani na watu wa dini nyingine sawa sawa wawe Mayahudi au Wakristo. 

Kwa nini Mashia wanatoa Salam za Krismasi kwa Wakristo?! | Pata jawabu maridhawa la swali hilo

Amesema: Hakika Mtume Muhammad (saww) alionesha mfano wa hali ya juu wa huruma, uvumilivu, na uadilifu kwa watu wote, wakiwemo Wakristo na Mayahudi.

Katika maisha ya Mtume wetu Muhammad (saww) ambaye ndiye Kiongozi wetu sisi kama Waislamu, bali Kiongozi wa walimwengu wote, tunapata mifano mingi ya uhusiano mwema na Wakristo, bali watu wote wasiokuwa Waislamu.

Mfano maarufu ni ule wa Mtume (saww) kuwapokea na kuwaheshimu Wakristo wa Najran walipokuja Madina, hata kuwaruhusu kufanya ibada yao Msikiti wakiwa Salama kwa Amani. 

Hali hii iliendelezwa na Imam Ali (as) na Maimamu wa Ahlul-Bayt (as), waliokuwa mfano wa haki, uadilifu na huruma kwa watu wote.

Kwa mantiki hiyo: Kuwapongeza Wakristo katika Krismasi yao, si kukubali itikadi zao, bali ni ishara ya heshima, utu na kuishi kwa amani, jambo ambalo linakuza maelewano na umoja katika jamii mchanganyiko. Hapana shaka kwamba: Akili timamu na maarifa sahihi ya Kiislamu yanahimiza hilo.

Kwa nini Mashia wanatoa Salam za Krismasi kwa Wakristo?! | Pata jawabu maridhawa la swali hilo

Ufafanuzi wa kina kuhusu uhusiano mwema kati ya Waislamu na Wakristo, kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (saww) na Ahlul-Bayt (as):

KUISHI KWA AMANI NA WAKRISTO: MSIMAMO WA UISLAMU KWA MTAZAMO WA MTUME (SAWW) NA AHLULBAYT (AS)

Maulana Sheikh Hemed Jalala, amebainisha kwamba: Uislamu umejengwa juu ya msingi wa huruma, haki, na amani. 

Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie yeye na Aali zake) alikuwa mfano bora wa kuishi kwa wema na watu wote, bila kujali dini zao. 

Kwa nini Mashia wanatoa Salam za Krismasi kwa Wakristo?! | Pata jawabu maridhawa la swali hilo

Katika maisha yake, aliweka uhusiano mzuri na Wakristo na Mayahudi, na kuwaheshimu kama wanadamu walioumbwa na Mwenyezi Mungu.

Moja ya mifano mashuhuri ni mapokezi aliyowapa Wakristo wa Najran walipokuja Madina. Mtume (saww) aliwakaribisha, akawapa heshima, na hata kuwaruhusu kufanya ibada zao Msikitini wakiwa salama. 

Hili linaonesha wazi kuwa Uislamu unahimiza kuheshimu imani za wengine, bila kuvunja misingi ya itikadi ya Kiislamu.

Kwa nini Mashia wanatoa Salam za Krismasi kwa Wakristo?! | Pata jawabu maridhawa la swali hilo

Viongozi wa nyumba ya Mtume, yaani Ahlulbayt (as), waliendeleza njia hii ya uadilifu. Imam Ali (as) katika utawala wake alitenda haki kwa wasiokuwa Waislamu kwa usawa, na alisisitiza kuwa wao pia wana haki chini ya serikali ya Kiislamu. Alisema: "Wao ni ndugu zetu katika ubinadamu."

Katika roho hii ya mafundisho, Mashia, wanaoifuata Ahlulbayt (as), wanaelewa kuwa kuishi kwa amani na Wakristo, Mayahudi, na watu wa dini nyingine ni sehemu ya maadili ya Kiislamu. Kuwapongeza Wakristo katika siku yao ya Krismasi ni ishara ya heshima na udugu wa kibinadamu — si kukubali itikadi yao, bali kuonesha utu na mshikamano wa kijamii.

Kwa nini Mashia wanatoa Salam za Krismasi kwa Wakristo?! | Pata jawabu maridhawa la swali hilo

Mtazamo huu unasisitizwa pia na akili na maarifa salama. Hakika, mtu yeyote mwenye elimu ya kweli ya Uislamu atakiri kuwa dini hii haifundishi chuki, bali hufundisha uadilifu, huruma, na kuishi kwa amani na kila mmoja.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha