Mwendesha Mashtaka wa Tehran ametangaza mashtaka dhidi ya baadhi ya wanasiasa kwa tuhuma za kushirikiana na Marekani na utawala wa Kizayuni, ambapo watu 4 wamekamatwa kwa madai ya kuchochea vurugu na kudhoofisha usalama wa ndani.
Maafisa wa Lebanon wameripoti kwamba angalau watu 32 wamekamatwa kwa tuhuma za kushirikiana na Mossad na kupeleka taarifa za kina kuhusu nafasi na harakati za Hezbollah kwenda Israel wakati wa vita vya hivi karibuni.