Makao Makuu ya Khatam al-Anbiyaa (s) yamesema vikosi vya Jeshi la Iran na Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu vimeshambulia baadhi ya kambi za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, vikieleza kuwa hatua hiyo ni jibu kwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran.
Kiongozi wa Mapinduzi amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika maandamano ya tarehe 22 Bahman na kuonyesha utii kwa Jamhuri ya Kiislamu ni silaha muhimu ya kuwarudisha nyuma maadui wanaolenga Iran na maslahi ya taifa. Amefafanua kuwa nguvu ya taifa haitokani zaidi na makombora au ndege za kivita, bali inatokana na umoja, fikra, azma na msimamo thabiti wa wananchi.