Umoja wa Falme za Kiarabu

  • WSJ Yadai UAE Ilifanya Mashambulizi ya Anga Dhidi ya Iran Wakati wa Vita

    WSJ Yadai UAE Ilifanya Mashambulizi ya Anga Dhidi ya Iran Wakati wa Vita

    Ripoti ya Wall Street Journal imedai kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu ulifanya makumi ya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran kuanzia siku za mwanzo za vita na kuendelea hadi baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano mwezi Aprili, madai yaliyoibua mjadala kuhusu nafasi ya mataifa ya Ghuba katika mzozo huo.

  • Araqchi: Umoja wa ardhi na mamlaka ya Yemen lazima vilindwe

    Araqchi: Umoja wa ardhi na mamlaka ya Yemen lazima vilindwe

    Katika mazingira ya kuongezeka kwa mvutano wa kisiasa na kijeshi nchini Yemen, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi, amesisitiza ulazima wa kulindwa umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo, akionya dhidi ya madhara ya mgawanyiko na kuingilia masuala ya ndani. Kauli hiyo imetolewa kupitia mazungumzo ya simu na mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, huku pia akigusia hali ya usalama nchini Yemen na kulaani uchokozi unaoendelea wa Israel dhidi ya Lebanon.

  • Waandamanaji London wakemea kuhusika kwa nchi za Magharibi katika vita vya Sudan

    Waandamanaji London wakemea kuhusika kwa nchi za Magharibi katika vita vya Sudan

    Waandamanaji walibeba mabango na kuziba baadhi ya barabara wakitaka hatua za haraka za kimataifa kuchukuliwa. Baadaye maandamano hayo yalizingira mgahawa wa OWO, ambapo baadhi ya wabunge wa Uingereza waliripotiwa kuwa na kikao, kabla ya kumalizika kwa amani kufuatia kuwasili kwa Polisi.