Kampuni ya CinnaGen ya Iran imepata mafanikio makubwa baada ya dawa yake ya Zandoriah (teriparatide) kuidhinishwa kuuzwa katika nchi 27 za Umoja wa Ulaya pamoja na nchi tatu za EEA, hatua inayochukuliwa kuwa mafanikio muhimu kwa sekta ya dawa na teknolojia ya afya ya Iran.
Orban ameonya kuwa tishio la Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia linazidi, na kwamba “waliberali wa Ulaya wanaounga mkono vita” wanapinga mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Russia.
Umoja wa Ulaya unakusudia kumuwekea vikwazo Abdulrahim Dagalo, Naibu Kamanda wa Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) nchini Sudan, kwa tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu.