Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema vitendo vya Israel havikuvuruga maslahi ya Iran na Lebanon, bali vimeimarisha mshikamano na kuongeza nguvu za Mhimili wa Muqawama katika kukabiliana na Israel.
“Katika vita vya siku 12, taifa la Iran bila shaka liliwashinda Marekani na utawala wa Kizayuni. Wao walikuja kufanya uhalifu na uovu, lakini waliadhibiwa na wakarudi mikono mitupu, bila kufikia malengo yao hata moja - na hilo ni kushindwa kwao kwa hakika.”