Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Palestina, Hamas, siku ya Ijumaa ilitangaza kuwa kura ya turufu (veto) ya Marekani dhidi ya azimio kuhusu Gaza ni uthibitisho wa wazi na kamili wa ushirikiano wake katika uhalifu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina walioko Ukanda wa Gaza.
Hamas imesema kuwa hatua hiyo inaonesha kuwa Marekani inasaidia moja kwa moja mashambulizi, mauaji na uharibifu unaofanywa na Israel dhidi ya raia wasio na hatia, na siyo tena mpatanishi wa haki katika mgogoro huo.
Vilevile, harakati hiyo imeitaka jumuiya ya kimataifa kusimama imara dhidi ya upendeleo huu na kuchukua hatua za dharura kuwalinda Wapalestina na kukomesha uvamizi wa Israel.