Afisa mstaafu wa jeshi la Marekani amesema Iran haipaswi tena kuiamini Marekani. Lawrence Wilkerson: “Kama ningekuwa Iran, nisingekubali tena kufanya mazungumzo na Washington.” Ameonya kuwa sera za Marekani zimejaa usaliti na kuziamini huleta gharama kubwa.
Mmoja wa maulamaa mashuhuri wa Kishia nchini Pakistan amesema kuwa usaliti wa Uturuki, baadhi ya nchi za Kiarabu na washirika wao umeacha majeraha makubwa yasiyoweza kupona katika mwili wa Palestina.