Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Jawad Naqvi, Kiongozi wa Harakati ya Uamsho wa Umma wa Mustafa nchini Pakistan, amekosoa msimamo wa serikali ya Pakistan kuhusu Israel, akisisitiza kuwa siasa za nchi hiyo za ubabaishaji zinapaswa kukoma.
Amesema kuwa viongozi wa Pakistan, kwa upande mmoja, hutoa kauli kali dhidi ya Israel, lakini kwa upande mwingine wanashirikiana na nchi zinazoiunga mkono Israel badala ya kuunga mkono ipasavyo makundi ya mapambano kama vile Hamas, Ansarullah ya Yemen, Iran na Hezbollah.
Naqvi ameongeza kuwa watawala wa Pakistan hata huwazuia Waislamu wa Kishia kufanya ziara za ardhini kwa kuwapachika jina la “Zainabiyoun”; hali ambayo ameieleza kuwa ni unafiki na siasa za upande mbili zinazopaswa kukomeshwa mara moja.
Amesisitiza kuwa haki haiwezi kuangamizwa na dhulma moja kwa moja, bali husambaratishwa kwa usaliti. “Kama vile Bani Umayyah walivyoshindwa kumpiga vita Mtume (s.a.w.w) moja kwa moja lakini wakaupiga Uislamu pigo lisilorekebishika kupitia unafiki na njama, vivyo hivyo leo Marekani, Israel na Ulaya hawajafanikiwa kuiteka Palestina kikamilifu; ila usaliti wa Uturuki, baadhi ya Waarabu na washirika wao umeiacha Palestina ikiwa na majeraha makubwa yasiyotibika.”
Alim huyo ameeleza kuwa hali ya sasa ya Gaza ni matokeo ya usaliti huo, na akasisitiza: “Iwapo watawala wa Kiarabu leo wataamka, bado inawezekana kugeuza hali ilivyo.”
Your Comment