Alexander Dugin, mwanafalsafa na mwananadharia wa kisiasa wa Urusi, akitoa maoni yake kuhusu kushindwa kwa Warepublican katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa Bunge la Marekani, aliandika katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X:
“Ni kweli kabisa. Iran imeshinda na Baal ameshindwa.”
Sheikh Ali Al-Khatib, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Waislamu wa Kishia nchini Lebanon, amesisitiza kuwa makabiliano na utawala wa Kizayuni wa Israel si mapambano ya kijeshi pekee, bali ni mapambano ya kistaarabu, kiutamaduni na kihistoria. Ameeleza kuwa, licha ya adui huyo kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka mataifa mbalimbali duniani, ameshindwa kuwalazimisha wananchi wa Lebanon kusalimu amri.