Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, amesema Baraza la Usalama linapaswa kuunga mkono diplomasia na kuepuka hatua zinazoweza kuchochea mvutano au kudhoofisha mazungumzo yanayoendelea.
Balozi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitawahi kusalimu amri mbele ya vitisho, mashinikizo au vitendo vya kutisha kutoka nje, akisisitiza kuwa taifa hilo litaendelea kulinda uhuru na haki zake kwa uthabiti.
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema jamii ya kimataifa inashuhudia kuongezeka kwa migogoro, ukosefu wa usawa na kudhoofika kwa diplomasia, huku akisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria za kimataifa na kuimarisha ushirikiano wa kweli wa kimataifa.