Rais alisema: “Mafanikio haya ni uthibitisho wa uwezo wa vijana na wataalamu wa Kiirani ambao, licha ya vikwazo vya kigeni, wameweza kuendeleza miradi mikubwa ya nyuklia kwa manufaa ya mwanadamu.”
Rais wa Shirika la Nishati ya Atomiki ya Iran katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Mionzi kaskazini-magharibi mwa nchi, alieleza kwamba teknolojia ya nyuklia ni tasnia ya kisasa, na matumizi ya mionzi ni hatua muhimu katika kuboresha afya na usalama wa chakula nchini. Pia alisisitiza kuwa teknolojia hii inaweza kuleta baraka nyingi kwa wananchi wa Iran.