Makubaliano ya kudhibiti biashara ya silaha duniani yanaanza kutekelezwa leo, huku wanaharakati wakiapa kuwa watahakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa ipasavyo.
Vladimir Putin raisi wa Urusi yuko ziarani India kuzungumzia ushirikiano wa kibiashara na nishati,katika wakati ambapo vikwazo vya nchi za magharibi vinatishia kuzorotesha shughuli za kiuchumi nchini mwake.
Rais wa China Xi Jinping amesema amefanya mazungumzo yenye tija na Rais wa Marekani Barack Obama na nchi hizo mbili zimekubaliana kuharakisha mazungumzo kuhusu uwekezaji wa pamoja na kuboresha uhusiano wa kijeshi.