Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Ivan Gil Pinto, amempongeza Iran kwa maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu, akisisitiza udugu na mshikamano wa nchi hizo mbili na kuthibitisha dhamira ya kuimarisha ushirikiano wa pamoja kwa ajili ya dunia ya pande nyingi, haki ya kijamii na amani ya mataifa.
Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amesema mbele ya mahakama ya New York kuwa yeye ni mfungwa wa vita, akisisitiza kuwa hana hatia na hakubali mashtaka yote yanayomkabili yeye na mkewe. Mahakama imeruhusu wawili hao kuwasiliana na ubalozi wa nchi yao, huku wakili wa Maduro akibainisha kuwa kwa sasa hawajaomba dhamana lakini wanaacha uwezekano huo wazi baadaye.