3 Juni 2025 - 17:02
Rais wa Baraza la Wawakilishi la Iran Awasilisha Zawadi ya Familia ya Shahidi Soleimani kwa Rais Maduro wakati wa Ziara Caracas

Rais wa Bunge | Baraza la wawakilishi la Iran akutana na Rais Maduro Caracas, na kumkabidhi sanamu ya Jenerali Shahidi Qasem Soleimani, iliyotumwa na familia ya Shahidi Soleimani kama zawadi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlulbayt (as) -ABNA- Mwishoni mwa ziara ya siku mbili ya Rais wa Bunge la Iran, Dk. Mohammad Baqer Qalibaf, mjini Caracas, siku ya Jumatatu (tarehe 1 Juni 2025), alikutana na kuzungumza na Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro.

Mkutano huo uliodumu dakika karibu 100, wawili hao walijadili njia za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kukuza biashara kati ya sekta binafsi.

Katika mkutano huo, Dk. Qalibaf alimkabidhi Rais Maduro sanamu ya Shahidi Qasem Soleimani, iliyotumwa na familia ya Shahidi Soleimani kama zawadi.

Familia ya Shahidi Soleimani walimkabidhi sanamu hiyo baada ya mahojiano ya Rais Maduro mwaka 2020, mara tu baada ya kifo cha Qasem Soleimani. Katika mahojiano hayo, Rais Maduro alitaja mchango wa Soleimani katika kupambana na ugaidi katika Asia Magharibi na kuhakikisha usalama wa nchi za eneo hilo. Pia alizungumzia usaidizi wa Soleimani kwa Venezuela wakati wa shambulio la mtandao lililotekelezwa na Marekani dhidi ya miundombinu ya Venezuela na kusema:
“Alikuja Venezuela, tukazungumza, na alitimiza kila ahadi yake ya kusaidia watu wa Venezuela dhidi ya shambulio hilo la mtandao. Ninamshukuru Mungu kwa kukutana na mtu huyu shujaa.”

Rais Maduro alionyesha shukrani zake kwa zawadi hiyo na kutoa pongezi zake kwa familia ya Shahidi Soleimani wakati wa mkutano huo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha