Rais wa zamani wa Venezuela Nicolás Maduro na mkewe, Cilia Flores, wameiomba mahakama ya Marekani kutupilia mbali mashtaka ya usafirishaji wa dawa za kulevya, wakidai kuwa wana kinga dhidi ya mashitaka ya jinai kutokana na hadhi yao kama kiongozi na mke wa kiongozi wa nchi ya kigeni.
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kukamatwa kwa Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mkewe katika operesheni maalum, akisema walihamishiwa New York kukabili mashtaka ya jinai, huku akisisitiza kuwa Marekani itaendelea kuhusika katika mustakabali wa Venezuela na kupambana na biashara ya dawa za kulevya.