Financial Times limeonya kuwa hatua yoyote ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran inaweza kusababisha vifo vya wanajeshi wa Marekani na kuathiri siasa za ndani pamoja na kampeni ya Donald Trump, huku uwezo wa mashambulizi makali ukitajwa kuwa mdogo na wa muda mfupi.
Kabul imeanza safari ya kuzalisha megawati 10,000 za umeme baada ya kusaini makubaliano makubwa zaidi ya nishati katika historia yake, mpango unaoweza kuibadilisha kutoka nchi inayoagiza umeme hadi kuwa muuzaji wa nishati katika ukanda.
Nchi za Kiarabu, ziko katika unyonge na haziwezi kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuathiri moja kwa moja utawala wa Kizayuni, na hivyo kuashiria kukosekana kwa ushirikiano wa kipevu na hatua thabiti dhidi ya Israel.