26 Juni 2025 - 22:18
Komenti ya mtumiaji wa Twitter (X)| "Hata baada ya bilioni moja ya miaka, Waarabu hawangeweza kufanya jambo kama hili!"

Nchi za Kiarabu, ziko katika unyonge na haziwezi kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuathiri moja kwa moja utawala wa Kizayuni, na hivyo kuashiria kukosekana kwa ushirikiano wa kipevu na hatua thabiti dhidi ya Israel.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mtumiaji mmoja wa Twitter ametoa mtazamo wake kuhusu WAARABU. Ametoa mtazamo huo kwa kukomenti katika posti ya Sayyid Ali Khamenei akisema:

"Hata baada ya bilioni moja ya miaka, Waarabu hawangeweza kufanya jambo kama hili!"

Mtazamo wake unaashiria kutoamini kuwa Waarabu wataweza kushirikiana au kuchukua hatua madhubuti dhidi ya Israel katika kipindi kijacho, labda kutokana na mtindo wa kisiasa wa sasa na hali ya uongozi katika baadhi ya nchi za Kiarabu ulivyo. 

Komenti ya Kiarabu | "Hata baada ya bilioni moja ya miaka, Waarabu hawangeweza kufanya jambo kama hili!"

Inaonekana wazi kuwa mtumiaji huyo wa X (zamani: Twitter) aliyekomenti chini ya Post ya Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, anaamini kabisa kuwa kwa sasa, nchi pekee ya Kiislamu yenye nguvu, na uwezo mkubwa wa Kijeshi, bali Ujasiri wa kumkabili adui Mzayuni na Marekani, ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (na Washirika wake), iliyoweza kuisambaratisha Makao Makuu ya Kijasusi ya Israel kwa jina "MOSSAD", ama nchi nyingine nyingi za Kiarabu ni dhaifu kupindukia, na ni vibaraka tu wa Israel.

Kwa Mantiki hiyo nchi za Kiarabu, ziko katika unyonge na haziwezi kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuathiri moja kwa moja utawala wa Kizayuni, na hivyo kuashiria kukosekana kwa ushirikiano wa kipevu na hatua thabiti dhidi ya Israel.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha