Mwakilishi mwenye mamlaka kamili wa Ayatollah Sistani nchini Iran amesema kuwa Arbaeen ni fursa kubwa sana kwa wasimamizi na wenye dhamana wa tukio hili la kimataifa, na hawapaswi kupuuzia au kughafilika na thawabu na malipo makubwa yanayopatikana kutokana nalo.
Mamlaka ya mahakama ya Lebanon siku ya Ijumaa ilimwachilia kwa masharti Hannibal Gaddafi, mwana wa Muammar Gaddafi, baada ya kuweka dhamana ya dola milioni 11.
Jaji husika katika Jumba la Mahakama la Beirut alimfikisha Hannibal mahakamani kwa mara ya kwanza tangu alipokamatwa.