Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa juhudi za Pakistan katika kuimarisha amani katika eneo la Mashariki ya Kati na Asia zina mizizi katika utamaduni wake tajiri, akisisitiza uhusiano wa karibu na malengo ya pamoja kati ya Tehran na Islamabad.
Tarehe 11 Februari 2026, maelfu ya Wairani walikusanyika kuonyesha mshikamano wao na taifa na kuthibitisha kwamba Marekani ni adui wa Umma wa Kiislamu.
Tukio hili linaonyesha wazi kwamba mbinu za adui hazina nafasi mbele ya mshikamano wa wananchi wa Iran na jitihada za kuharibu taifa hilo hazina mafanikio.