Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina, kupitia taarifa yake, imelaani vikali mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya raia wa Kipalestina na wanaharakati wa kigeni katika msimu wa kitaifa wa uvunaji wa zeituni katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Harakati ya Upinzani ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa haina nia ya kushiriki katika mipango ya utawala wa ukanda wa Gaza baada ya kuisha kwa mashambulizi ya utawala wa kikoloni, na imeitaka kuundwa kwa kamati ya usimamizi kwa makubaliano ya makundi yote ya Kipalestina.