Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amemjibu kwa ukali Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akisisitiza kuwa Iran bado ina mambo ambayo haijamalizana nayo na utawala wa Israel. Araghchi amesema kuwa jaribio la mwisho la Israel la kutaka kuiangamiza Iran liliifanya nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku akimtuhumu Netanyahu kwa kuisukuma Marekani katika vita vingine ili kuepuka kufungwa jela.
Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, amesema Baraza la Usalama linapaswa kuunga mkono diplomasia na kuepuka hatua zinazoweza kuchochea mvutano au kudhoofisha mazungumzo yanayoendelea.