26 Oktoba 2026 - 10:20
Araghchi Amjibu Netanyahu: Iran Pia Ina Hesabu Ambazo Bado Haijamalizana Nanyi!

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amemjibu kwa ukali Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akisisitiza kuwa Iran bado ina mambo ambayo haijamalizana nayo na utawala wa Israel. Araghchi amesema kuwa jaribio la mwisho la Israel la kutaka kuiangamiza Iran liliifanya nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku akimtuhumu Netanyahu kwa kuisukuma Marekani katika vita vingine ili kuepuka kufungwa jela.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amejibu matamshi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kumwonya dhidi ya kuendeleza vitisho na uchokozi dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu bado ina hesabu ambazo haijamalizana nazo na Israel.

Katika ujumbe aliouchapisha Jumapili jioni kupitia akaunti yake katika mtandao wa kijamii wa X, Araghchi alikosoa kauli za Netanyahu kuhusu kutaka kukamilisha kile alichokiita jukumu dhidi ya Iran.

Akijibu matamshi hayo, Araghchi aliandika:

"Mara ya mwisho mlipotaka 'kukamilisha kazi', Iran iliibuka ikiwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali. Je, mnataka kujaribu bahati yenu tena? Karibuni, lakini jihadharini; sisi pia tuna hesabu ambazo bado hatujamalizana nanyi!"

Kauli hiyo ya Araghchi imekuja ikiwa ni jibu la moja kwa moja kwa matamshi ya Netanyahu, huku Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Iran akisisitiza kuwa vitisho vya Israel havijafanikiwa kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha, Araghchi amemtuhumu Netanyahu kwa kujaribu kuisukuma Marekani kuingia katika vita vingine, akidai kuwa lengo lake ni kukwepa hatari ya kufungwa jela kutokana na matatizo ya kisheria yanayomkabili.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Iran alisema:

"Netanyahu anaisukuma Marekani kuelekea katika vita vingine ili kuepuka kuingia jela, bila kujali madhara ya hatua hiyo kwa Israel, achilia mbali madhara yake kwa Rais wa Marekani."

Kwa mujibu wa kauli hiyo, Araghchi anaamini kuwa Netanyahu anatanguliza maslahi yake binafsi ya kisiasa na kisheria kuliko athari zinazoweza kujitokeza kutokana na kuanzishwa kwa vita vingine katika eneo la Mashariki ya Kati.

Matamshi hayo yanaonesha kuendelea kwa mvutano wa kisiasa na kidiplomasia kati ya Iran na Israel, huku Tehran ikisisitiza msimamo wake wa kupinga vitisho na hatua zozote za kijeshi zinazolenga usalama na mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha