Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amemjibu kwa ukali Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akisisitiza kuwa Iran bado ina mambo ambayo haijamalizana nayo na utawala wa Israel. Araghchi amesema kuwa jaribio la mwisho la Israel la kutaka kuiangamiza Iran liliifanya nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali, huku akimtuhumu Netanyahu kwa kuisukuma Marekani katika vita vingine ili kuepuka kufungwa jela.
Walinzi wa Mapinduzi wakiionya Uingereza:
“Tunauonya utawala wa kifalme wa Uingereza, ambao umekuwa sababu kuu ya mateso ya watu wa eneo letu, una historia nyeusi ya kugawanya nchi za Kiislamu na kuhusika katika mauaji makubwa katika nchi hizo, pamoja na kushiriki kwa kiwango kikubwa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, usifanye historia yake kuwa ya maangamizi na uovu mkubwa zaidi kuliko ilivyo.”