Ofisi ya Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa mwaka 2026 takribani watu milioni 22 — sawa na asilimia 45 ya watu wa Afghanistan — watahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu; huku idadi ya watu wenye uhaba mkali wa chakula ikifikia milioni 17.4 na milioni 5.2 wakiwa katika hatari ya njaa kali.
Katika taarifa yake ya hivi punde kuhusu tatizo la maji nchini Afghanistan, UNAMA ilisema kuwa zaidi ya watu milioni 10, karibu theluthi moja ya wakazi wa Afghanistan, hawana maji safi ya kunywa na wanatumia vyanzo vya maji visivyo safi.