Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran, Brigedia Jenerali Tala'inik, wizara hiyo imehamasisha uwezo wake wote katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad ili kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wanaoshiriki shughuli za mazishi ya kiongozi shahidi, ikiwemo huduma za kitabibu, kitamaduni na msaada wa kiutendaji.
Ripoti ya NBC imeeleza kuwa uwezekano wa kurejea kwa vita kati ya Marekani na Iran unakabiliwa na changamoto kubwa za kijeshi, kutokana na mabadiliko ya mkakati wa Iran wa kusambaza na kuficha uwezo wake wa kijeshi kwa kuhamisha silaha chini ya ardhi na kutumia mifumo ya rununu inayohamishika mara kwa mara.