Rais wa Lebanon, katika kikao chake na ujumbe wa Benki ya Dunia, alisisitiza kujitolea kwa nchi yake kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano, huku akilaani kuongezeka kwa uvamizi unaofanywa na utawala wa Kizayuni katika eneo la kusini mwa Lebanon. Aidha, aliomba taasisi za kifedha za kimataifa zitoe msaada kwa mchakato wa maendeleo na mageuzi nchini Lebanon.
Msafara wa Kimataifa wa Ustahimilivu (al-Sumud) umetangaza kuwa Jeshi la Majini la utawala wa Kizayuni limeushambulia Msafara wa Uhuru uliokuwa ukielekea Gaza kwa lengo la kuvunja mzingiro unaoendelea dhidi ya eneo hilo.