Katibu Mkuu wa Hezbollah amesema kuwa mpango wa kuangamiza Iran na muqawama umefeli, akisisitiza kuwa kusitishwa kwa mapigano lazima kuwe kwa masharti ya kusitishwa kabisa kwa uvamizi na kujiondoa kwa adui katika maeneo wanayoyakalia.
Mshauri wa kijeshi wa Kiongozi Mkuu wa Iran amesema Marekani itawajibishwa iwapo kutakuwa na tishio lolote dhidi ya Iran, huku ripoti zikieleza kuwa Tehran imekataa kurejea kwenye mazungumzo ya moja kwa moja, ingawa mawasiliano kupitia wapatanishi bado yanaendelea.
Israel tayari inatambua maana ya Dhulfiqar na imekwisha kuonja makali yake, huku Iran ikiwa imeapa kupigana na Israel vita vya mwisho endapo kutakuwa na shambulizi lolote toka kwa adui.