27 Januari 2026 - 21:37
Dhulfiqar: Kombora la Kivita la Iran Linaloashiria Makali ya Imam Ali (AS)

Israel tayari inatambua maana ya Dhulfiqar na imekwisha kuonja makali yake, huku Iran ikiwa imeapa kupigana na Israel vita vya mwisho endapo kutakuwa na shambulizi lolote toka kwa adui.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA- Kwa wale wanaojua, neno Dhulfiqar linahusiana na panga / upanga  wa kivita la Imam Ali bin Abi Talib (AS).

Kombora la Iran limepewa jina hilo kutokana na makali na uimara wake, ikionesha nguvu ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wale wanaojua historia ya makali ya upanga wa Sayyidna Ali (AS) wanaweza kuelewa wazi ukali na usahihi wa kombora hili.

Kombora la Dhulfiqar liko katika hali ya utayari wa operesheni, ili kuonyesha maana halisi ya jina lake endapo adui atakosea katoka hesabu zake, hata kwa tukio dogo la shambulizi linalolenga Ardhi ya Iran linaweza kupata majibu makali na ya kupelekea kujuta kwa adui.

Israel tayari inatambua maana ya Dhulfiqar na imekwisha kuonja makali yake, huku Iran ikiwa imeapa kupigana na Israel vita vya mwisho endapo kutakuwa na shambulizi lolote dhidi yake toka kwa adui.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha