Makubaliano ya amani kati ya Iran na Marekani yameibua mabadiliko makubwa ya kisiasa Mashariki ya Kati, huku yakionekana kuwa ushindi wa diplomasia lakini yakizua mvutano mpya kuhusu Lebanon, Israel na mustakabali wa uhusiano wa Washington na Tel Aviv.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Gharib Abadi, amesema nguvu za kijeshi za Iran ndizo zilizomlazimisha adui kurejea kwenye mazungumzo, akisisitiza kuwa maandishi ya mwisho ya hati ya maelewano yamekamilika na kutiwa saini rasmi kutafanyika Ijumaa nchini Uswisi, huku Iran ikiahidi kujibu hatua yoyote ya kutotekelezwa kwa ahadi za upande wa pili.
Rais wa Brazil Lula da Silva akizungumza katika mkutano wa kimataifa mjini New York Marekani amesisitiza juu ya ulazima wa kutatuliwa kwa amani suala la Palestina na kutekelezwa kwa mapatano ya serikali mbili.