Ujumbe wa Iran mjini Vienna umesema kuwa azimio la Baraza la Magavana la IAEA dhidi ya Iran ni la kisiasa na lisilo la kitaalamu, ukisisitiza kuwa Tehran itajibu hatua hiyo ili kulinda haki zake zisizoweza kuondolewa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa wale wanaotumia machafuko kama njia ya kutawala mataifa mengine huishia kuwa watumwa wa machafuko hayo. Ameonya kwamba nguvu iliyoundwa kwa ajili ya kuwatawala wengine hatimaye huweza kutoka katika udhibiti wa walioiunda.