Ayatollah Al-Udhma Abdullah Javadi Amoli alisisitiza umuhimu wa kuunganisha sanaa na ushairi na Tauhidi (umoja wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu), akisema kuwa iwapo mafundisho ya tauhidi yatahuishwa kwa sura yake halisi, basi jamii ya Kiislamu haitapotea wala kukumbwa na vitisho kutoka kwa maadui.
Je, Hadhrat Ali (AS) alifanya nini wakati Mwanaume mmoja Mkristo aliposilimu? Kwa heshima ya kusilimu kwake, alimpa ngao yake (inayovaliwa vitani) na kumpa nafasi katika Serikali.