Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - ABNA - Wakristo daima wameichukulia Dini yao kuwa ni Dini ya wema, na wanawachukulia wazee wao na viongozi wao kuwa viongozi katika nyanja ya maadili. Hata hivyo, kwa kutazama juu juu Biblia Takatifu na zile Gospeli / Injili nne, mtu mwenye akili timamu na muungwana atatambua kwamba si viongozi wao tu bali pia hata mungu wao, Yesu Kristo - Issa bin Maryam - (amani iwe juu yake), - kwa mujibu wao kama wakristo - alionyesha ukosefu wake wa maadili na ukosefu wa fadhili katika hali mbalimbali.
Katika Injili ya Mathayo, inaelezwa kwamba Mwanamke Mgiriki alimwendea Yesu ili kumtafutia bintiye uponyaji, lakini badala ya Yesu kumfariji, Yesu alimjibu hivi: “Waache watoto (wa Bani Israil) washibe kwanza, kwa maana si sawa kuchukua mkate wa watoto na kuwatupia mbwa!"
Wakati wa Ukhalifa wa Imam Ali (a.s) huko al-Kufa, ngao yake ya kivita ilipotea. Baada ya muda, ilipatikana ikiwa na Mwanamume Mkristo. Imam Ali (amani iwe juu yake) akampeleka kwa hakimu na akafungua kesi ya madai kwamba silaha (ngao) hii ni yangu, sijaiuza wala sijampa mtu yeyote, na sasa nimeipata kwa mtu huyu.
Hakimu akamwambia Mkristo: Khalifa ameeleza madai yake, wewe unasemaje? Mkristo yule akasema: Ngao hii ni yangu, na wakati huo huo, sikatai na sikadhibishi Makamu ya Ukhalifa (inawezekana kwamba Khalifa amekosea). Hakimu akamgeukia Imam Ali (amani iwe juu yake) na kusema: Wewe ndiye mdai na mtu huyu ndiye mwenye kukanusha, kwa hiyo ni juu yako kuleta shahidi juu ya madai yako. Ali (amani iwe juu yake) alicheka na kusema: Hakimu yuko sahihi, sasa hivi ilitakiwa Mimi ndio nilete Mashahidi, lakini Mashahidi sina. Kutokana na Imam Ali (a.s) kukosa kukosa Shahidi wa kumtetea na kuthibitisha madai yake mbele ya hakimu, Hakimu aliamua kumpendelea Mkristo huyo, kwa kuzingatia kanuni kwamba mlalamikaji hakuwa na Mashahidi, hivyo Mkristo yule akachukua ngao ile na kuondoka zake.
Mwanaume yule Mkristo, ambaye alijua zaidi pasina shaka yoyote kuwa Ngao ile mali ya nani, baada ya kutembea hatua chache, dhamiri yake ilitetemeka na akarudi nyuma. Na akasema: “Mtindo huu (Tabia hii na Mwenendo huu) wa utawala kwa hakika sio Mwenendo na sio aina ya tabia ya Mwanadamu wa kawaida, bali hii ni aina ya Serikali ya Manabii,” na akakiri kwamba Ngao hii ni mali ya Ali bin Abi Talib (amani iwe juu yake). Baada ya kukiri ile ni ngao ya Imam Ali (a.s), Imam Ali (a.s) aliamua kumzawadia Mkristo huyo ngao hiyo na sasa akaimiliki kihalali. Na haikuchukua muda mrefu kwake kusilimu na kisha akaenda kupigana vita kwa shauku na imani chini ya bendera ya Imam Ali (amani iwe juu yake) katika vile Vita vya Kihistoria vya Nahrawan.
Kilichomfanya Mkristo yule kusilimu kwa haraka na hata kuamua kuingia katika vita vya Nahrawan akiwa chini ya Jeshi la Imam Ali (a.s), ni hukumu ya kiuadilifu aliyokutana nayo katika kipindi cha Ukhalifa na Serikali ya Kiislamu aliyoiongoza Imam Ali bin (a.s). Na kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda kuona uadilifu ukitendwa kwa Waja Wake, na Mwenyezi Mungu ni Muadilifu na huwapenda sana waadilifu katika waja wake.
-
Chanzo:
Imam Ali, Saut al-Adalah al-Insaniyah (الامام علي، صوت العدالة الانسانیة، صفحه ۶۳) , Ukurasa wa 63.
Your Comment